Picha haihusiani na shule husika
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Pugu mkoani Dar es Salaam, wanadaiwa kupata anemia kutokana na kuumwa na kunguni waliojikita kwenye samani na kila mahali kwa miongo kadhaa.
Hali hiyo, imesababisha wazazi na wanafunzi kuulaumu uongozi wa shule hiyo kushindwa kuwaangamiza wadudu hao wanaowanyonya damu watoto hadi kusababisha maradhi ya upungufu wa damu.
Hata hivyo, katika hali ya kuonyesha kutojali, uongozi wa shule unasema kunguni ni kitu kidogo siyo tatizo la kupasua kichwa.
0 comments:
Post a Comment