Godfrey Mgimwa akiwa ameshika hati ya ushindi na mkewe Roby Mgimwa
Katika
uchaguzi huo uliofanyika Jumapili ya Machi 16, mwaka huu, Mgimwa alizoa kura
22, 962 ambazo ni sawa na asilimia 79.32 dhidi ya kura 5,853 sawa na asilimia
20 alizopata Grace Tendega wa Chadema na kura 150 sawa na asilimia 0.52
alizopata Richard Minja wa Chausta.
Msimamizi
wa uchaguzi huo Pudenciana Kisaka ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Iringa jana alimkabidhi Mgimwa hati yake ya kuchaguliwa kuwa mbunge
wa jimbo hilo.
Godfrey Mgimwa
Akizungumza
na wanahabari baadaye Mgimwa alisema anazikumbuka ahadi zote alizotoa kwa
wananchi wa jimbo hilo wakati wa kampeni zake na anajipanga kutekeleza moja
baada ya nyingine.
“Kama
mnavyojua nyingi ya ahadi hizo zitatekelezwa kupitia Ilani yetu ya CCM;
nachowahakikishia wananchi wangu wawe na imani kwani mambo yatatekelezwa,”
alisema huku akiwashukuru wapiga kura wa jimbo hilo kwa kumpa ushindi wa
kishindo dhidi ya wapinzani wake.
Pamoja
na Chadema kuleta wabunge wake wote siku tatu kabla ya uchaguzi huo na kutumia
chopa kwenye kampeni zake kabla ya kuitumia kulinda kura siku ya uchaguzi, Mgimwa
alimgaragaza mgombea wa Chadema hata katika kata zilizokuwa zikielezwa kuwa ni
ngome ya chama hicho.
Kata
hizo ni pamoja na Ifunda ambayo Mgimwa alipata jumla ya kura 1,627 dhidi ya 601
alizopata mgombea wa CCM na 13 za mgombea wa Chausta.
Nyingine
ni Nzihi ambayo CCM ilipataa kura 1,793 dhidi ya 606 za Chadema na saba za
Chausta.
Katika
kata ya Magulilwa ambako mgombea wa Chadema ndiko anakotokea, Mgimwa alifanya
vizuri zaidi kwa kupata kura 2,065 dhidi ya kura 549 za Chadema.
Matokeo
ynayofana na hayo yalitokea pia katika kata zingine zote za jimbo hilo; wakati
Mgimwa akipata kati ya kura 1,500 na 3,000, mgombea wa Chadema alipata kati ya
kura 200 na 700 tu.
CHANZO:Bongo leaks
0 comments:
Post a Comment