Home » » VIONGOZI WA CHADEMA MAKETE WAMWAGWA

VIONGOZI WA CHADEMA MAKETE WAMWAGWA

Written By kitulofm on Tuesday, 11 March 2014 | Tuesday, March 11, 2014

Aliyekuwa mwenyekiti wa CHADEMA (W) ya Makete Shaban Mkakanze akiwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA taifa Dr.Wilbroad Slaa

Chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kimefikia hatua ya kuchukua maamuzi magumu baada ya kuufuta uongozi wote wa ngazi ya wilaya ya Makete, na kuuingiza uongozi wa muda ili kukinusuru chama hicho

Hatua hiyo imefikiwa baada ya mkutano wa wanachama uliofanyika jumamosi machi 8, mwaka huu kwa pamoja kuazimia kuung'oa madarakani uongozi uliokuwepo baada ya kujadiliana kwa kina katika mkutano huo

Miongoni mwa viongozi waliong'olewa ni pamoja na mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Makete Bw. Sahaaban Mkakanze na katibu wake pamoja na uongozi mzima uliokuwa ukiongoza chama hicho wilaya

Mkutano huo ambao pia uliowashirikisha viongozi wa chadema mkoa wa Njombe akiwemo mwenyekiti Bw. Lulandala, ulibaini kuwa kasi ya kukua kwa chama hicho wilayani Makete ni ndogo ukilinganisha na maeneo mengine licha ya jitihada zinazofanywa na ndiyo maana wakaona wabadilishe uongozi

Katika mkutano huo waliazimia kuchagua uongozi wa muda ambao umepewa miezi miwili ya matazamio kuhakikisha wanakiimarisha chama katika kata zote za wilaya ya Makete ikiwemo kuunda uongozi wa kila kata ambao unaweza kufanya kazi kama inavyotakiwa

Viongozi wa wa muda waliochaguliwa kushikilia chama hicho ngazi ya wilaya kwa muda ni Bw. Ibrahim Ngogo ambaye ni mwenyekiti, Bw. Ilomo ambaye ni katibu na Bw. Stephano Kasanga ambaye ni katibu mwenezi

Mkutano huo umewapa miezi miwili ya kukiimarisha chama kabla ya kuitishwa mkutano mwingine ambao utakuwa wa uchaguzi wa wanachama kuwachagua viongozi wa wilaya wa kukiongoza chama hicho.

Na Edwin Moshi, Makete.
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

KITULO FM LOGO

KITULO FM LOGO
Tusikilize masaa 18 kwa siku kupitia masafa ya 97.0 FM ukiwa wilayani Makete mkoani Njombe na maeneo ya jirani

WASOMAJI WETU

KUMBUKUMBU YA HABARI ZETU

 

Copyright © 2013. KITULOFM BLOG - Haki zote zimehifadhiwa
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inawezeshwa na Kitulo Fm