Home » » WANAFUNZI 500 WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA WAINGIA MITINI WILAYANI ROMBO

WANAFUNZI 500 WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA WAINGIA MITINI WILAYANI ROMBO

Written By kitulofm on Tuesday, 11 March 2014 | Tuesday, March 11, 2014

Baadhi ya wanafunzi wa Sekondari katika moja ya shule za Wilaya ya Rombo wakiwa darasani.
Baadhi ya wanafunzi wa Sekondari katika moja ya shule 
za Wilaya ya Rombo wakiwa darasani.

Yohane Gervas, Rombo
ZAIDI ya wanafunzi 500 waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2013 ambao wangetakiwa kuanza kidato cha kwanza mwaka huu (2014) hadi sasa bado hawajaripoti katika shule walizopangiwa.

Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Elinasi Pallengyo amesema kuwa kati ya wanafunzi 558 waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza hadi sasa bado hawajaripoti shuleni kati yao ni wasichana 265 na wavulana 293. 

Alisema kuwa idadi hiyo ni kubwa na hivyo serikali katika Wilaya ya Rombo, inaendelea kufanya jitihada za kuhakikisha wazazi waliogoma kuwapeleka wanafunzi shuleni wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vinavyohusika.

Aidha Pallengyo alisema kuwa kutokana na hali ya utoro wa wanafunzi wa kidato cha kwanza kuzidi kuongezeka halmashauri ya Wilaya ya Rombo imedhamiria kutunga sheria ndogo ya kusimamia elimu ya sekondari. 

Pia katika hatua nyingine Mkuu huyo wa wilaya amewataka wananchi wilayani humo kutumia vizuri mvua za masika zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali wilayani Rombo kupanda mazao ya muda mfupi na mazo mengine yanayostahimili ukame.
Chanzo.eddy blog
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

KITULO FM LOGO

KITULO FM LOGO
Tusikilize masaa 18 kwa siku kupitia masafa ya 97.0 FM ukiwa wilayani Makete mkoani Njombe na maeneo ya jirani

WASOMAJI WETU

KUMBUKUMBU YA HABARI ZETU

 

Copyright © 2013. KITULOFM BLOG - Haki zote zimehifadhiwa
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inawezeshwa na Kitulo Fm