Home » » CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA NJOMBE (NPC) CHAPITISHA KATIBA YA CHAMA HICHO

CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA NJOMBE (NPC) CHAPITISHA KATIBA YA CHAMA HICHO

Written By kitulofm on Wednesday, 30 October 2013 | Wednesday, October 30, 2013

Wajumbe wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Njombe, Njombe Press Club (NPC) hivi karibuni wameipitisha katiba ya chama hicho katika mkutano mkuu uliofanyika katika ukumbi wa Dosmeza mkoani Njombe

Hatua hiyo imetokana na wajumbe hao wakiongozwa na mwenyekiti wa NPC Mercy James na katibu Hamis Kassapa, kupitia hatua kwa hatua kila kipengele kilichopo kwenye katiba hiyo ili chama hicho kizidi kufanya kazi kwa uimara zaidi

Kupitishwa kwa katiba hiyo kumezidi kukiimarisha chama hicho kizidi kufanya kazi zake chini ya misingi ya kisheria ya chama na nchi kwa ujumla

Katika hatua nyingine chama hicho kwa pamoja kimedhamiria kuwa mialiko ya shughuli mbalimbali hasa za kiserikali zikiwemo ziara za viongozi mbalimbali, kupitia kwenye chama na si vinginevyo kutokana na kuwepo kwa mikanganyiko ya waandishi wa habari ambao ni wanachama kwenda kienyeji kwenye shughuli mbalimbali bila idhini ya chama

Aidha wamesema wataandika barua kwa taasisi mbalimbali kuzitaarifu kuhusu suala hilo ili lianze mara moja

Na Edwin Moshi
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

KITULO FM LOGO

KITULO FM LOGO
Tusikilize masaa 18 kwa siku kupitia masafa ya 97.0 FM ukiwa wilayani Makete mkoani Njombe na maeneo ya jirani

WASOMAJI WETU

KUMBUKUMBU YA HABARI ZETU

 

Copyright © 2013. KITULOFM BLOG - Haki zote zimehifadhiwa
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inawezeshwa na Kitulo Fm