WAGANGA
wawili wa jadi akiwemo mfanyabiashara mmoja wamenaswa jijini Mwanza
wakiwa na kiungo cha mkono wa kulia unaoamainika kuwa wa binaadamu
ambapo walikamatwa kwenye eneo la ziwani na Uwanja wa Ndege wa Mwanza,
kufatia taarifa za raia wema na kisha jeshi la polisi kuweka mtego kwa
muda wa wiki nzima na kufanikiwa kuwakamata.
Kaimu
Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza Joseph Konyo amethibitisha tukio hilo
na kwamba mkono huo uliokuwa umewekwa kwenye begi ukiwa umefungwa kwenye
mfuko mweusi wa plasitiki na kuviringishwa kwenye karatasi nyeupe ya
nailoni, umekutwa ukiwa mbichi.
======
======
Konyo
ambaye pia ni Mkuu wa Upelelezi wa makosa ya jinai mkoani Mwanza (RCO),
alieleza kuwa watuhumiwa hao (majina yanahifadhiwa) wenye umri wa miaka
36 na 43 (ni waganga wa jadi wawili) na mfanyabiashara ana miaka 48.
Taarifa zilizotolewa katika jeshi hilo na kuweka mtego huo kisha makubaliano ya kununua viungo hivyo kutoka kwa watuhumiwa hao (wauzaji), walimhakikishia mnunuzi (polisi) kuwa wanaweza kupata kichwa, mikono, miguu na sehemu za siri za binaadamu endapo mteja angehitaji.
kwa mujibu wa makubaliano hayo wauzaji hao ambao ni Waganga walitaka kupewa shilingi milioni 100 kwa mkono huo mmoja lakini baada ya kufanya mazungumzo ya kibiashara na wao kuona kitita cha fedha, walilegeza bei na kujikuta wakitiwa mbaroni

0 comments:
Post a Comment