Home » » JAMAA AJIKATA UUME WAKE BAADA YA MADEMU KUMKATAA KWA KIPINDI KIREFU

JAMAA AJIKATA UUME WAKE BAADA YA MADEMU KUMKATAA KWA KIPINDI KIREFU

Written By kitulofm on Wednesday, 30 October 2013 | Wednesday, October 30, 2013

Jamaa mmoja nchini China ameukata uume wake mara baada kuchukizwa na hali ya kutokuwa na demu kwa kipindi kirefu, na mara baada ya kitendo hicho jamaa alikimbizwa hispitali kwa matibabu.

Alipofikishwa hospitali madaktari walimueleza wasingeweza kumsaidia sababu kipande cha uume alioukata kiliachwa sehemu ambayo alilifanya tendo hilo, hivyo ikaamuliwa arudi nyumbani kwake akakichukue ili aweze kupata matibabu.

Yang Hu, 26, alifanikiwa kurudi tena hospitali, huku akiwa na watu kadhaa, madaktari walimueleza kwamba kipande kilichokatwa kilipoteza damu nyingi sana hivyo ingeshindikana kuweza kukiunga tena.

Marafiki wa Yang walisema kila kukicha jamaa alikuwa anatingwa sana na mawazo kutokana na ukweli kwamba toka alipohamia jijini hapo hakuwahi kupata demu.

Mbaya zaidi, walisema, jamaa alikuwa akifanya kazi kwa masaa mengi kwenye kiwanda cha nguo ndani ya Jiaxing, kwenye jimbo la Zhejiang Mashariki ya China, huku wakihisi kuwa ndiyo kitu kilichomsababisha kutokuwa na muda wakukutana na mwanamke.

Msongo kichwani ulizidi kuongezeka kwa kasi, kiasi cha kumfanya kuzidi kujisikia vibaya zaidi, mnamo tarehe 27 Oktoba mara baada ya kurudi nyumbani majira ya saa 3 usiku jamaa alikodi chumba na kuamua kuukata uume wake kutokana na kuona kwamba hakikuwa ni kitu cha maama na hakikuwa na faida naye, huku akiamini kitendo hicho kingeweza kumsaidia kuacha kufikiria juu ya maswala ya mademu
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

KITULO FM LOGO

KITULO FM LOGO
Tusikilize masaa 18 kwa siku kupitia masafa ya 97.0 FM ukiwa wilayani Makete mkoani Njombe na maeneo ya jirani

WASOMAJI WETU

KUMBUKUMBU YA HABARI ZETU

 

Copyright © 2013. KITULOFM BLOG - Haki zote zimehifadhiwa
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inawezeshwa na Kitulo Fm