Nchi za Kiafrika zimeyataka mataifa makubwa duniani kuwa na utashi
wa kisiasa katika kutekeleza ahadi za misaada ya kifedha
itakayoziwezesha nchi zinazoendelea kukabiliana na athari za mabadiliko
ya tabia nchi.
Akihutubia katika mkutano wa 19 wa umoja wa mataifa kuhusu
mabadiliko ya tabia nchi mjini warsaw nchini poland, rais wa jamhuri ya
muungano wa tanzania ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya marais wa
afrika kuhusu mabadiliko ya tabia nchi mh jakaya kikwete,amesema pamoja
na kuwa bara la afrika linazalisha kiasi kidogo cha hewa ukaa bara hilo
limekuwa ni muathirika mkuu wa athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia
nchi hivyo ni budi nchi tajiri kulihakikishia bara la afrika vyanzo vya
uhakika na endevu vya fedha,teknolojia pamoja na ujuzi wa kukabiliana na
athari hizo.
Aidha rais kikwete amesema kuwa ni matarajio ya nchi za kiafrika
kuwa mkutano wa poland utatoka na maamuzi ya msingi ikiwa ni pamoja na
kuweka utaratibu wa kushughulikia hasara na athari zitokanazo na
mabadiliko ya tabaia nchi.
Kwa upande katibu mkuu wa umoja wa mataifa bwana ban ki moon
amesema maafa yanayotokea hivi sasa katika maeneo mbalimbali ya dunia
akitolea mfano maafa ya hivi karibuni nchini ufilipino ni matokeo ya
athari za mabadiliko ya tabia nchi na kuongeza kuwa jitihada za
kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi ni ndogo
ikilinganishwa na athari ambazo dunia imeanza kuzishuhudia na hivyo
nguvu za ziada zinahitajika.

0 comments:
Post a Comment