Watu wawili raia wa China ambao ni viongozi wa kiwanda cha Urafiki
plastick kinachotengeneza mifuko ya aina mbalimbali eneo la Mabibo
jijini Dar es Salaam,wameshikiliwa na jeshi la polisi kwa kudaiwa
kufukia kiganja cha mkono wa mfanyakazi wao uliokatwa na mashine za
kiwanda hicho siku ya Jumapili usiku.
ITV ilifika katika eneo la Mabibo jijini Dar es Salaam pembezoni
mwa kiwanda cha urafiki plastick na kukuta watu wakiwa wanashangaa tukio
la kufukiwa kwa kiganja hicho,ambapo ndugu wa bwana Jumanne Rashid
ambaye amedaiwa kuwa ni mfanyakazi wa kiwanda hicho,wamesema ndugu yao
alikatwa na mashine katika kiwanda hicho siku ya Jumapili usiku na
wamiliki wa kiwanda hicho walipoulizwa wakadai mkono wa kijana huyo
ilisagika kabisa hali iliyosababisha kijana huyo bwana Jumanne Rashid
kulazwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili mpaka sasa.
Jitihada za ITV kuzungumza na raia hao wa China kuhusu tukio hilo
ziligonga mwamba baada ya raia hao wa kigeni kudai kutokuwa na uwezo wa
kuzungumza kiswahili wala kiingereza na hivyo kushikiliwa na maafisa wa
polisi kisha kuondoka na kiganja hicho,ambapo ili kupata taarifa za
hospitali ya taifa ya Muhimbili alikolazwa kijana aliyekatwa mkono
zilishindikana baada ya afisa uhusiano wa hospitali hiyo bwana Aminieli
Eligaesha kutopokea simu akidai yupo katika mkutano huku mkurugenzi
mtendaji wa hospitali hiyo dakta Marina Njelekela alipopigiwa simu
alijibu yupo safarini nchini Marekani huku kamanda wa polisi mkoa wa
Kipolisi Kinondoni ACP Camilius Wambura amethibitisha kukamatwa kwa
kiganja hicho na kusema tayari kijana aliyekatwa mkono katika kiwanda
hicho amehojiwa katika hospitali ya Muhimbili na wafanyakazi wa kiwanda
hicho
CHANZO:ITV
0 comments:
Post a Comment