Home »
» AKAMATWA NA SARE ZA JWTZ JIJINI MBEYA
Jeshi la polisi mkoani Mbeya linamshikilia Peter Patrick (20) mkazi wa
Sae jijini hapo kwa tuhuma za kukutwa na sare za Jeshi la Wananchi wa
Tanzania (Jwtz).
Kaimu kamanda wa Polisi mkoani Mbeya kamishna
msaidizi Robart Malaya alisema kuwa tukio hilo lilitoa oktoba 31 mwaka
huu saa 5:00 usiku maeneo ya Mamajohn.
Aliendelea kwa kusema kuwa mtuhumiwa alikutwa amevaa kofia,kombati na
buti la jeshi hilo kitu ambacho ni kinyume na sheria na taratibu
zinafanywa ili kuweza kufikishwa mahakamani kujibu mastaka yanayo
mkabili.
Na Saimeni Mgalula,Mbeya
0 comments:
Post a Comment