Mkuu wa Mkoa wa Njombe Captain Mstaafu Asseri Msangi Akiwakagua wanafunzi wa Shule ya Msingi Ninga Leo.
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Captain Mstaafu Asseri Msangi Ameuagiza Uongozi wa Kata ya Ninga Kufuatilia Wanafunzi Wote Wanaoshindwa Kusoma na Kuandika Pamoja na Watoro Katika Shule ya Msingi Ninga Kufuatia Kuwepo kwa Wanafunzi Wanaokariri Miaka Mingi.
Agizo Hilo Amelitoa Leo Wakati wa Ziara yake ya Siku Tatu Katika Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Ambapo Pamoja na Mambo Mengine Alifanya Ziara ya Kushtukiza Katika Shule Hiyo na Kubaini Baadhi ya Wanafunzi Kushindwa Kusoma na Kuandika Hali Inayopelekea Kurudia Darasa Miaka Mingi.
Aidha Kaptain Mstaafu Asseri Msangi Amesema Uongozi wa Kata Hiyo ni Lazima Uwakutanishe Wazazi wa Watoto Hao Pamoja na Walimu Ili Kufanya Uchunguzi wa Kina Unaosababisha Kufeli Kwa Wanafunzi Hao na Kutoroka.
Katika Hatua Nyingine Captain Mstaafu Msangi Ameagiza Kila Shule Ihakikishe inaweka Shelfu za Vitabu Kwa Kila Darasa Kwani Serikali Ipo Mbioni Kugawa Vitabu vya Kutosha Kila Shule Ambapo Matunzo Makubwa ya Vitabu Hivyo Yanahitajika.
Mbali na Hayo Lakini Pia Amesema Suala la Uhaba wa Madawati Katika Shule za Msingi na Sekondari Mkoani Njombe Haliwezi Kuvumilika Kutokana na Mkoa Kuzalisha Kwa Wingi Zao la Mbao na Kuliuza Katika Mikoa Mingine na Nchi Jirani.
Hatua hiyo imekuja baada ya kubaini Wanafunzi Sita Kukaa Kwenye Dawati Moja katika Shule ya Msingi Ninga Katika Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Leo.
Na Gabriel Kilamlya Njombe.
0 comments:
Post a Comment