
Msanii kutoka Uganda Bebe cool
Msanii wa muziki kutoka nchini Uganda, Bebe Cool ameweza kuiwakilisha vizuri nchi yake huko Zimbabwe
ambapo katika mpambano wake na msanii D'Banj kutoka Nigeria, msanii huyu kutoka Uganda aliweza kufanya onyesho kali lililomfunika hasimu wake huyo.
Tukio hili ni kutoka tamasha la Battle For Africa ambalo liliwakutanisha wakali hawa wa muziki, na mwisho wa siku Bebe Cool akaweza kufunika kutokana na kile kilichotajwa kuwa nyimbo zake kuwa kipenzi cha mashabiki wengi wa muziki kutoka nchini humo.
Kwa upande wa D Banj, ripoti zinaweka wazi kuwa staa huyu aliweza kufanya poa katika dakika 45 za kwanza za onyesho lake, na baadaye mambo kumbadilikia kutokana na mashabiki kutokuwa na ufahamu mkubwa wa nyimbo
0 comments:
Post a Comment