MAKETE
Wafanyabiashara wa mkaa
Wilayani Makete mkoani Njombe Wanakabiliwa na changamoto kubwa ya wateja wa
mkaa huo kuwa wasumbufu pindi wanunuapo mkaa
Wameyasema hayo mapema hii
leo walipo kuwa wakizungumza na kitulo fm eneo la sokoni Makete mjini ambapo
wauzaji hao wanafanyia biashara hiyo
Wamesema kuwa wanakerwa sana na tabia ya wateja walio wengi kuambiwa
wabebe mkaa huo kwa umbali mrefu hadi majumbani kwao pasipo kupewa fedha yoyote
mbali na fedha ya mkaa
Wafanyabiashara hao wamesema
kuwa fedha ya kununulia mkaa ni vema ingelikuwa tofauti na fedha ya kubebea
mkaa huo.
Aidha wafanyabiashara hao
wamezungumzia kuhusu kushuka kwa bei ya mkaa kutoka Sh.10,000-5000 kwa gunia
0 comments:
Post a Comment