Wini Madikizela aliyekuwa mke wa rais mstaafu wa Afrika kusini Nelson Mandela ametoa taarifa kwa vyombo vya habari kuwa hali ya rais wa zamani wa Afrika kusini Nelson Mandela ni mbaya na hawezi kuzungumza
Taarifa hiyo inasema kuwa kwa sasa
Mandela anaongea kwa kutoa ishara tu na sauti yake haitoki na kwa kiasi
kikubwa anategemea mipira aliyowekewa akiwa anaendelea na matibabu
nyumbani
Madaktari nchini humo wameahidi kuendelea kupambana na hali hiyo ya mandela hadi sauti yake irudi kama mwanzoni
Kwa sasa Mzee Mandela anaendelea na matibabu yake akiwa nyumbani kwake nchini Afrika kusini

0 comments:
Post a Comment