Na Verinica Mtauka
Makambako
Tunajali inatarajia kuzindua mradi mkubwa wa ZIRO VVU katika mikoa ya Iringa na Njombe katika kutokomeza maambukizi ya ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto
Hayo yamebainishwa mjini Makambako kwenye warsha kwa wadau wa habari na wanahabari wa vyombo vya habari mkoa wa Njombe na Iringa ambapo wahabari hao wametakiwa kuwa chachu kwa kutumia vyombo vya habarikatika kutoa elimu kuhusu tiba ya ART kwa maisha yote kwa wajawazito na wanaonyonyesha wenye VVU
Katika kikao hicho imebainika kuwa Tanzania imepiga hatua kubwa katika kupunguza viwango vya maambukiziya virusi vya ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtotohadi kufikia mwaka 2010 asilimia 94 ya vituo vya afya ya uzazina mtotovilikiwa vinatoa hudumakuzuia maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto na kufikia takribani asilimia 70 ya wajawazito walio katikatiba ya kuzuia maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto


0 comments:
Post a Comment