Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana, akihutubia maelfu ya wananchi katika Uwanja wa Shule ya
Msingi Mwaka, mjini Tunduma, wilayani Momba, jioni hii, Nov 28, 2013,Kinana
ameitaka Serikali kupunguza ama kuwaondolea vikwazo wananchi katika suala
zima la kujiletea maendeo yao,pia ameongoza kuwa Viongozi wawasikilize Wananchi
badala ya kuka maofisni na semina kila wakati ambazo hazina tija yoyote kwa
wananchi,Ndugu Kinana na ujumbe wake yupo katika ziara ya kukagua utekelezaji
wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kuzungumza nao njia ya
kuzitatua, katika mkoa wa Mbeya.
Sehemu ya umati wa watu waliofurika kwenye mkutano huo wa hadhara
wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ambaye aliwakonga nyoyo
wakazi wa eneo hilo wakiwemo wapinzani kwa kusema kuwa hatakuwa tayari
kuwavumilia viongozi wanaoshindwa kutatua kero za wananchi,waliojawa na
umangimeza na urasimu.
Katibu wa NEC, Siasa na Uhisiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro
(katikati mwenye miwani) akiserebuka
na wananchi kwenye mkutano, Uwanja wa shule ya Mwaka, Tunduma jana
Katibu wa NEC,
Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano mkubwa wa hadhara
uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi katika uwanja wa shule ya msingi Mwaka
mjini Tunduma wilayani Momba mkoani Mbeya
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha
Rose Migiro, akihutubia katika mkutano huo,ambapo alisisitiza kuweka
kipaumbele cha elimu kwa watoto wa kike pamoja kupiga vita unyanyasaji wa
wanawake na watoto.






0 comments:
Post a Comment