Home » » MATATIZO NA MAZINGIRA YA CHUO CHA SHUKRANI IDYDC KILICHOPO WILAYANI MAKETE

MATATIZO NA MAZINGIRA YA CHUO CHA SHUKRANI IDYDC KILICHOPO WILAYANI MAKETE

Written By kitulofm on Monday, 4 November 2013 | Monday, November 04, 2013



Chuo cha shukurani IDYDC (Iringa development of youth disabled people&children care) kilichopo wilayani makete kinakabiliwa na changamoto  mbalimbali ikiwa ni pamoja na wanafunzi walio wengi  kukatisha masomo yao  na kurubuniwa na wafanya biashara katika mikoa ya  jirani na kwenda kufanya biashara mbalimbali mikoani humo .

Hayo yamesemwa mapema hii leo na Mratibu wa IDYDC Bw.Godrey Mwautwa alipokuwa akizungumza na kitulo fm ofisini kwake.

Pamoja na changamoto hiyo ya wanafunzi hao kurubuniwa na wafanya biashara kutoka mkoani mbeyana mkoani Njombe hayo huwakuta wanafunzi hao pindi wanapokuwa wameenda likizo hawarudi tena chuoni na ndipo imegundulika kuwa wanalubuniwa na watu hao

Pia chuo hicho kilianza kutoka mafunzo mwaka 2005 wilayani makete ambapo idadi ya wanafunzi waliosajiliwa kujiunga na chuo hicho kwa mwaka 2013/2014 ni 75 lakini mpaka sasa ni wanafunzi 40 tu waliopo chuoni hapo

Aidha malengo ya chuo hicho ni kutoa wahitimu 50 kila mwaka

Ambapo chuo hicho kinakabiliwa na tatizo la kutokuwa na majengo ya kudumu kwani wanafanya kazi katika majengo ya kupangisha,hakina wafadhiri wa kuwasaidia sehemu maaluma ya kutendea kazi kitu ambacho kinafanya washindwe kuendelea mbele na katoa wito kwa wazazi kuwa na ushirikiano. 

Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

KITULO FM LOGO

KITULO FM LOGO
Tusikilize masaa 18 kwa siku kupitia masafa ya 97.0 FM ukiwa wilayani Makete mkoani Njombe na maeneo ya jirani

WASOMAJI WETU

KUMBUKUMBU YA HABARI ZETU

 

Copyright © 2013. KITULOFM BLOG - Haki zote zimehifadhiwa
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inawezeshwa na Kitulo Fm