Mtu mmoja ambaye ni mkazi wa kijiji cha Ivalalia kata ya Iwawa wilayani Makete amefariki dunia baada ya kudondokewa na kifusi cha mchanga wakati akichimba mchanga
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Mkuu wa upelezi wilayani Makete Bw.Gozbert Komba amemtaja mkazi huyo kuwa ni Daudi Ilomo (42)amesema kuwa amefariki dunia wakati akichimba mchanga kijijini hapo
Aidha ameongeza kuwa marehemu ameongeza kuwa marehemu amekutwa akiwa amevunjika mguu mara mbili,pia alitokwa na damu puani na masikioni baada ya kifusi hicho kumbana katika mwili wake hasa kifuani
Hata hivyo marehemu wakati wa uhai wake na kwa mara ya mwisho alikuwa na Bw.Polito ilomo
Pia ametoa wito kwa wananchi wote kuwa makini pindi wanapokuwa katika maeneo wanaojua kuwa ni hatarishi kwao kuwa katika makundi ili kusaidiana na kujiepusha katika majanga kama ya aina hiyo
Home »
» MTU MMOJA AUWAWA KWA KUFUKIWA NA KIFUSI MKAZI WA IVALALILA WILAYANI MAKETE
MTU MMOJA AUWAWA KWA KUFUKIWA NA KIFUSI MKAZI WA IVALALILA WILAYANI MAKETE
Written By kitulofm on Friday, 8 November 2013 | Friday, November 08, 2013
Related Articles
If you enjoyed this article just click here, or subscribe to receive more great content just like it.
0 comments:
Post a Comment