Home » » POMBE YATUMIKA KUWAITA WAUMINI KANISANI

POMBE YATUMIKA KUWAITA WAUMINI KANISANI

Written By kitulofm on Monday, 4 November 2013 | Monday, November 04, 2013

Kanisa moja la jimboni Texas nchini Marekani lijulikanalo kwa jina la Church-in-a-Pub limeamua kuwavutia waumini wapya kutoka nyanja mbalimbali za kimaisha kwa kutumia pombe.

Huduma hiyo inadhaminiwa na Mchungaji Philip Heinze wa kanisa lale la Kilutheri la Calvary.

Viongozi, waumini na wasio waumini kila mmoja anashindwa kutafsiri mantiki ya mpango huo ambao Mch. Heinze anasema
haulengi katika kujipatia waumini wengi bali kuwavutia watu wawe katika mahusiano na Yesu na kama itabidi kutumia bia, yeye haoni tatizo.

Viongozi wakuu wa Baraza la Kanisa la Kiinjili la Kilutheri la Marekani walikataa kukubaliana na mwenendo huo lakini baadaye walitangaza kuwa Church-in-a-pub sasa inaruhusiwa na Sinodi kuwa jumuiya ya washarika. Mwaka ujao, itamtaka mchungaji kijana aeneze wazo hilo katika maeneo mengine ya Dallas-Fort Worth.

Nako huko katika viunga vya Portland jijini Oregon (Marekani pia), katika kanisa la zamani la First Christian huwa wanafungua ukumbi wao kwa ajili ya sherehe ya "Bia & Tenzi" ambapo hupata mahudhurio ya watu takriban 100, wengi wao wakiwa vijana ambao hujipatia bia zilizotengenezwa na waumini na kugawiwa kwenye vikombe kwa kiwango cha ukomo wa vikombe viwili kwa mtu mmoja.

Pengine bia/pombe Kanisani si jipya, kwa mfano, soma: 5 Things You Might Not Have Known About God And Beer.

Ikiwa huu ni mkondo mpya na wa kudumu wa kuwavutia watu Kanisani au ni jambo la kupita tu, hakuna ajuaye kwa sasa kwani mkondo wa kufumuka kwa madhehebu katika dini mbalimbali huanza kwa namna waonavyo wahusika ni sawa.
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

KITULO FM LOGO

KITULO FM LOGO
Tusikilize masaa 18 kwa siku kupitia masafa ya 97.0 FM ukiwa wilayani Makete mkoani Njombe na maeneo ya jirani

WASOMAJI WETU

KUMBUKUMBU YA HABARI ZETU

 

Copyright © 2013. KITULOFM BLOG - Haki zote zimehifadhiwa
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inawezeshwa na Kitulo Fm