Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Wadau mbali mbali
walioshiriki kwenye Warsha ya Kamata Fursa Twenzetu,iliyofanyika leo
kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,jijini Dar es Salaam.
Mh. Rais
ameupongeza uongozi wa Kampuni ya Clouds Media Group kwa ubunifu wao wa
Kampeni ya Fusra inayowakutanisha na kuwahamasisha vijana mbali mbali
nchini kujituma na kufanya kazi ili kutokomeza swala zima la ukosefu wa
ajira,Pia Rais Kikwete ameahidi kuwasaidia waendeshaji wa Warsha
hiyo.Picha zote na Othman Michuzi.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Clouds Media Group,Joseph Kusaga akizungumza
machache kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi,Rais Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete,ili aweze kuzungumza na Wadau mbali mbali walioshiriki kwenye
Warsha ya Kamata Fursa Twenzetu,iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa
Diamond Jubilee,Jijini Dar es Salaam.


0 comments:
Post a Comment