Wananchi wa kijiji cha
Utweve,Masisiwe kata ya Ukwama na Usagatikwa kata ya Tandala wilayani Makete wanaendelea na
ujenzi wa kuunganisha barabara kati ya vijiji hivyo ulioanza mwaka 2011
Akizungumza na kitulo fm
Mwenyekiti wa kijiji hicho Bw.Lauten Enock Sanga amesema kuwa shirika la TASAPH
ndilo lililowataka wananchi wa vijiji hivyo kuibua mradi wowote na wananchi hao
wakaamua kutengeneza barabara itakayo viunganisha vijiji hivyo
Amesema mradi huo gharama
zote ni nguvu za shirika hilo
ambapo walianza ujenzi wa barabara hiyo mwaka 2011 ikiwa hadi sasa mkakati wa
ukamilishaji wa kuweka makaravati katika barabara hiyo unaendelea
Hata hivyo amelishukuru
shirika la TASAPH kwa jitihada hizo kwani itasaidia hata kukuza kiwango cha
uuzaji wa mazao na kurahisisha usafiri kati ya vijiji jirani hivyo na kuongeza
kuwa wananchi wameupokea kwa mikono miwili mradi huo ambapo pia umetoa ajira
kwa wakazi wa vijiji kwa kufanya kazi za kukwetua,kufenya nyasi pamoja na
kuchimba barabara hiyo.
Na Furahisha Nundu
0 comments:
Post a Comment