Home » » WANAWAKE MAKETE WAPEWA NGURUWE

WANAWAKE MAKETE WAPEWA NGURUWE

Written By kitulofm on Monday, 18 November 2013 | Monday, November 18, 2013




MAKETE

Umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi kata ya isapulano wamekabiziwa mradi wa nguruwe wenye thamani ya shilingi laki mbili na themanini  kutoka kwa Mh.diwani wa kata ya Isapulano Aginiwe Mahenge kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo la Makete

Akikabidhi nguruwe hao kwa niaba ya mbunge Binilith Mahenge ambaye ni mbunge wa jimbo la Makete amewataka wana kikundi hicho kutunza nguruwe hao ili kuendelea kuongeza kipato ili waweze kujikwamua kwenye wimbi la umasikini.

Kwa upende wake muwakilishi wa kikundi hicho Bi. Etelinah Mahenge amemshukuru Mh. mbunge kwa kutoa msaada huo na kuahidi kuwa watautunza mradi huo kwa hali na mali ili kuongeza kipato katika maisha yao.

Nguruwe hao wametolewa na mh. mbunge wa makete ikiwa ni ahadi yake aliyoitoa tarehe kumi na tano septemba mwaka huu wakati wa ziara yake kijiji hapo. 

Na Riziki Manfred
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

KITULO FM LOGO

KITULO FM LOGO
Tusikilize masaa 18 kwa siku kupitia masafa ya 97.0 FM ukiwa wilayani Makete mkoani Njombe na maeneo ya jirani

WASOMAJI WETU

KUMBUKUMBU YA HABARI ZETU

 

Copyright © 2013. KITULOFM BLOG - Haki zote zimehifadhiwa
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inawezeshwa na Kitulo Fm