Naibu mkuu wa usalama wa taifa nchini Libya Mustafa
Noah ametekwa nyara nje ya uwanja wa ndege wa
kimataifa mjini Tripoli.
Mustafa Noah hakuwa na walinzi
wakati alipokamatwa na hakuna kundi hadi sasa
lililodai kuhusika na tukio hilo.
Viongozi wa mji wa
Tripoli jana walitoa wito wa kufanyika maandamano na
migomo kwa wenye maduka, shule na vyuo vikuu
kuilazimisha serikali ya Libya kuyaondoa makundi ya
wanamgambo.
Makundi hayo yanalaumiwa kwa kuhusika
katika mapigano siku ya Ijumaa na Jumamosi ambapo
watu 46 wameuwawa.
0 comments:
Post a Comment