
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein ameutaka uongozi wa Chuo
Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kuhakikisha kuwa upanuzi wa mitaala,
ufundishaji na tafiti zinazofanywa na chuo hicho zinaelekezwa katika
kutoa michango na rai zitakazochangia na kurahisisha utekelezaji wa
mipango ya maendeleo ya nchi.
Akizungumza wakati wa mahafali ya tisa ya Chuo Kikuu hicho
yaliyofanyika jana huko Tunguu, mara baada ya kuwatunuku vyeti,
stashahada na shahada wahitimu 763, Dk. Shein amesema ni jukumu la vyuo
vikuu hasa vya serikali kutoa taaluma inayolenga kurahisisha utekelezaji
wa mipango ya maendeleo taifa na jamii kwa ujumla.
Alisema zitihada zinazofanywa na chuo za kukuza elimu zitakuwa na
manufaa zaidi endapo elimu itakayotolewa italiongoza Taifa na itatumika
kurahisisha maisha na kuimarisha maendeleo kwa kusaidia utekelezaji wa
Dira ya Maendeleo 2020, MKUZA II, Malengo ya Milenia na Ilani ya
Uchaguzi ya CCM.
0 comments:
Post a Comment