Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Njombe na
mjumbe wa NEC Taifa Bi.Pindi Chana ametoa kiasi cha sh.milioni moja laki
4,majembe,vitenge pamoja na karenda kwa viongozi wa UWT Wilaya ya Makete kwa
lengo la kuwaendeleza akina mama wa Makete kiuchumi.
Akizungumza na baraza UWT Wilaya ya Makete Bi.Pindi Chana amesema akina mama wananafasi kubwa ya
kuleta maendeleo katika jamii na
hivyo kama Taifa litaelekeza nguvu kwa
akina mama umasikini unaweza kufika
kikomo.
Kwa upande wake Katibu wa UWT Wilaya ya Makete Bi.Safi Almasi
amevitaja vitu vilivyotolewa kuwa ni pamoja na fedha zilizo tolewa
na Bi.Chana na kuongeza kuwa kiongozi huyo amekuwa ni mfano wa kuigwa hapa nchini na wilayani Makete
Katika baraza hilo pia
kulihudhuliwa na mjumbe wa Chama Cha Mapinduzi (w)Bw.Ona Sukunala Nkwama ambaye pia amemshukuru Mh.Pindi Chana kwa kuwajali wanawake nchini ikiwa
ni pamoja na kuwatembelea katika wilaya ya Makete
0 comments:
Post a Comment