
Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu utaratibu wa kupata majina ya
wajumbe watakaoteuliwa kwenye Bunge la Katiba. Picha na Fidelis Felix.
- Ni wa kuwapata wajumbe kutoka makundi mbalimbali kuingia kwenye Bunge la Katiba.
Vyama vya siasa,
wafanyakazi, walemavu na makundi mengine ya watu maalumu, leo wanaanza
mchakato wa uteuzi wa majina ya watu wanaotaka kuomba nafasi ya
kuchaguliwa kuingia kwenye Bunge la Katiba.
Kwa mujibu wa taarifa ya Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe aliyoitoa mwishoni mwa wiki, ilisema mpaka kufikia Januari 2 mwakani, majina ya watu hao yanatakiwa kuwa yamefika mahali husika ili uteuzi uanze kufanyika.
Kwa mujibu wa Chikawe, makundi hayo yanajumuisha wajumbe 20 kutoka taasisi zisizokuwa za kiserikali na nusu yao lazima wawe wanawake na moja ya tatu watatoka Zanzibar.
Pia wajumbe 20 watatoka taasisi zote za dini, wajumbe 42 kutoka vyama vyote vya siasa vyenye usajili wa kudumu.
Kwa mujibu wa mchanganua huo, kati ya vyama 21 kila chama kitatoa wajumbe wawili na kwamba kwa vyama vya siasa ni lazima mjumbe mmoja atoke Zanzibar na mmoja awe mwanamke na mwingine mwanamume.
Wajumbe wengine wanatoka taasisi za Elimu ya Juu watakuwa (20), makundi ya watu wenye ulemavu (20), vyama vya wafanyakazi (19), vyama vinavyowawakilisha wafugaji (10), vyama vinavyowawakilisha wavuvi (10) na vyama vya wakulima (20). Katika nafasi hizo, pia zimetengwa 20 kwa ajili ya wajumbe kutoka makundi mengine yenye malengo yanayofanana.
Pia wajumbe 20 watatoka kwenye taasisi zisizokuwa za kiserikali na nusu yao lazima wawe wanawake.
CHANZO:Blog ya Wananchi
0 comments:
Post a Comment