Suala
la machine zinazomilikiwa na Mamalaka ya Mapato
Tanzania[Tra]zimeendelea kuwasumbua wafanyabiashara mbalimbali,baada ya
88.5 Kariakoo Dar kugoma na 87.8 Mbeya nao kugomea uwepo wa hizi mashine
sasa ni 88.1 Mwanza nao wamegomea hizi mashine
Wafanyabiasha
wa maduka ya jijini Mwanza leo wagoma kufungua maduka yao wakigomea
mashine za kutolea risiti za EFD toka TRA,maduka mengi mitaa mbalimbali
ya Mwanza hayajafunguliwa hizi ni baadhi ya picha za maeneo mbalimbali
jijini Mwanza.
Wafanyabiashara
walikutana kituo cha zamani cha mabasi cha Tanganyika wakiwa na mabango
mbalimbali yanayowasilisha ujumbe wa kupishana na mashine hizo ambapo
mbali na makato yake pia kodi nyingine hutozwa pembeni hali
wanayoitafsiri kama unyonyaji.

0 comments:
Post a Comment