KIJANA Adam Mtaki (20) amelazwa katika hosptali ya mji mdogo wa Tunduma
wilayani Momba mkoa wa Mbeya,baada ya kupata kipigo na kufanyiwa mateso
makali na watu wanaodaiwa kuwa askari Polisi wa kituo cha Tunduma.
Adamu ambaye ni mtoto wa tatu wa mwandishi wa habari wa kampuni
yaUhuru Publications LTD Shomi Mtaki anayeripoti kutokea mji wa Tunduma
uliopo mpakani mwa Tanzania na Zambia.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa baba mzazi wa kijana huyo, Shomi Mtaki
alisema kuwa tukio hilo limetokea Disemba 5 majira ya saa 5.00 usiku
eneo la mtaa Wasikanyika wakati Adam alipo kutana na watu wawili
wanaodaiwa kua ni askari polisi waliovalia nguo za kiraia ambapo mmoja
alimfahamu kwa jina moja la Shuku.
SOMA ZAIDI:AMINIA WEBSITE

0 comments:
Post a Comment