Sakata la baadhi ya wabunge kutuhumiana kuwa wamechukua fedha za serikali kwa ajili ya kufanya Safari na hawakusafiri limechukua sura nyingine baada ya spika wa bunge Mh. Anne Makinda kuwataka wale wote waliochukua fedha hiizo bila ya kusafiri wazirudishe na huku akisisitiza anawajua wote kwa majina.
Mh Makinda ameyasema hayo alipokuwa akiongoza mkutano wa kumi na nne na kikao cha kumi na tisa ambapo amesema anashangazwa na maneno maneno ambayo wabunge wamekuwa wakitupiana wakati anawajua wote waliochukua fedha bila ya kusafiri.
0 comments:
Post a Comment