Waandamanaji Ukraine wakiwa katika mitaa mbali mbali.
Waandamanaji hao pia walizuia wafanyakazi kuendelea na shughuli zao
wakishinikiza msukumo mpya kudai rais Viktor Yanukovich ajiuzulu
kutokana na mzozo wa uhusiano na Umoja wa Ulaya.
Maadamano hayo yamefutia mkaubliano ya wananchi kuitiisha maandamano ya
nchi nzima , ambapo walifunga njia kuu ya kuingilia kwenye majengo ya
serikali huku wakiwa wamebeba mabanko yenye jumbe mbali mbali.
Msemaji wa makamu wa rais wa nchi hiyo, Mykola Azarov amesema kuwa
wafanyakazi wameshindwa kuingia ofisini, huku wakifanya juhudi za
kuzungumza na waandamanaji hao kuwaruhusu wafanyakazi kuingia ofisini,
na kuwaeleza kuwa, rais Azarov alikuwa hajawasili kazini.
Maandamano hayo yalilenga majengo ya serikali baada ya maadamano ya
upinzani yaliyohusisha takribani watu 350,000 jana, katika mji mkuu wa
Ukraine, KIEV na kusababisha vurugu baina ya polisi na waandamanaji hao.

0 comments:
Post a Comment