Kijiji
hicho chenye zaidi ya wakazi 500 tokea kuanza kwake hakijawahi kuwa na barabara
za mitaa hivyo wameamua kuanza usembuaji wa barabara hizo,wazo hilo lilikuja mara baada
ya kuona kupata shida linapotokea tatizo la msiba wakati wa kwenda mazikoni
ndipo waliamua watengeneze barabara ili ziwarahishie kupita
Kitulo
imezungumza na Afisa Mtendaji wa kijiji hicho Bw.Bensony Mbilinyi ameelezea
changamoto iliyokuwepo baada ya kutokuwa na miundombinu ya barabara hizo hivyo
amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi pindi wanapotangaza siku na muda wa
kwenda kushirikiana ktk kazi hiyo
Kijiji
hicho chenye jumla ya vitongoji 6 kimeonekana kuwa na ushirikiano mkubwa kati
ya kitongoji na kitongoji hata hivyo kila kitongoji wanasembua barabara kutoka
kitongoji chao hadi kufikia kitongoji kingine
Na Furahisha Nundu
0 comments:
Post a Comment