Wananchi wilayani Makete
wameeleza changamoto mbalimbali kwa Mh.Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya
Makete Bw.Daniel Okoka ikiwemo kero ya Umeme kutoka Makete-Tandala,Miundombinu
ya barabara,Elimu,Afya pamoja na Redio kitulo fm kutofika katika baadhi ya
maeneo wilayani Hapa
Kero hizo zimetolewa na
wananchi usiku wa kuamkia leo katika kipindi cha Maalumu cha Twanga swali hapa
kitulo fm kilichodhaminiwa na Gazeti la Daraja lililopo Mkoani Njombe kipindi
hicho kiliochofanywa kuanzia saa 1:15 usiku hadi saa 3:20 usiku hapa kitulo fm
hapo jana
Kuhusu suala la Umeme kwa
wananchi wa Tandala hasa kitongoji cha Kilovoko amesema kuwa nguzo zimesimama
pamoja na nyaya,transfoma zimefungwa hivyo kinachosubiriwa ni mchakato wa
kuunganisha umeme katika Gredi ya Taifa kutoka Mbeya uliopo Makete mjini na
sasa zoezi hilo lipo ukingoni hivyo amewaomba wananchi kuwa na subira katika
hili kwani Mkandarasi anaendelea na kazi
Hata hivyo akijibu suala la
Barabara ya Lupila ameelezea mengi na kusema kuwa zaidi ya kiasi cha sh.milioni
27 katika fedha zilizotengwa za matengenezo ya barabara kwani hata hivyo fedha
hizo bado hazijatolewa hivyo mara baada ya kutolewa mapema ukarabati wa
barabara hiyo utaanza mapema
Kwa upande wa Kuboresha
masafa ya Redio Mh.Okoka amesema kuwa kuna mabadiliko mengi yaliyofanywa
ikiwemo kubadilisha uongozi wa Redio pamoja na vipindi vyake
kuimarishwa,wamefanya jitihada za kuunda bodi ya Redio ambayo wanauhakika
itasimamia kiuhakika shughuli zote na kuweza kuongeza chachu ya kukua kwa Redio
hata hivyo amesema kuwa kuna Mradi wa UNISEF kwa kushirikiana na Redio Clauds
Fm walianza kutoa msaada ili kuboresha hayo yote katika redio lakini kuna watu
wamehujumu kwa upande wa fedha hivyo kusababisha kukwama hivyo anataka andiko
maalumu kuhusu fedha hizo kwa watu waliohusika mara moja.
Na Furahisha Nundu
0 comments:
Post a Comment