Home » » WAKAZI WA JIMBO LA KALENGA MKOANI IRINGA WAMETAKIWA KUWA WATULIVU NA KUENDELEA KULINDA AMANI ILIYOPO KATIKA KIPINDI HIKI CHA KAMPENI

WAKAZI WA JIMBO LA KALENGA MKOANI IRINGA WAMETAKIWA KUWA WATULIVU NA KUENDELEA KULINDA AMANI ILIYOPO KATIKA KIPINDI HIKI CHA KAMPENI

Written By kitulofm on Tuesday, 25 February 2014 | Tuesday, February 25, 2014

IRINGA

Wakazi wa jimbo la kalenga,wilaya ya Iringa vijijini,mkoani Iringa wameombwa kuwa watulivu na kuendelea kuilinda amani iliyopo katika kipindi hiki cha kampeni zinzoendelea na kuelekea uchaguzi wa mbunge jimbo humo.

Katibu mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA,Dr Willbrod Slaa,amesema hayo wakati alipokuwa akifungua kampeni za ubunge za chama hicho,February 22 zilizofanyika kwenye viwanja vya ngome ya Mkwawa kata ya Kalenga,mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM mkoani iringa.

Dkt.Slaa ameongeza  kuwa mchakato wa kumpata mgombea ndani ya chama hicho ulifanyika ambapo mgombea alipatikana  baada ya kupigiwa kura na wajumbe zaidi ya 400,lakini alishindwa kutetea nafasi hiyo katika kura za wagombea wenyewe wapatao 13 na nafasi yake kuchukuliwa na Grace Tendega.

Aidha Dr Slaa ameongeza kuwa CHADEMA kitaendelea kusimamia suala la kuto ongezwa kwa posho ya sh.lakitatu inayodaiwa ni ndogo na baadhi ya wajumbe wa bunge la katiba ambapo mwenyekiti wa chama hicho yupo kwenye kamati tendaji ya kujadili suala hilo.

Naye mgombea wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Bi. Grace Tendega amesema wananchi ndio wenye jukumu la kumpima na kumchagua ambapo yeye atashughulikia changamoto za  jimbo hilo ikiwa ni pamoja na ukosefu na ucheleweshwaji wa pembejeo.

Kwa upande wa Chama Cha Mapinduzi wanaendelea na mikutano kwa maandalizi ya ufunguzi rasmi wa kampeni hizo ambazo wanatarajia kufungua februari 27 mwaka huu.

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ugwachanya kata ya Mseke jimboni humo februari 23,mwaka huu,Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa Bi.Jesca Msambatavangu,amesema vijana na wakazi wa jimbo hilo wasikubali kuingia kwenye vurugu zinazo fanywa na baadhi ya vyama vya siasa,na kuwataka watambue thamani ya amani iliopo kwa sasa hapa nchi.

Naye mgombea wa nafasi hiyo kupitia CCM Bw.Godfley Mgimwa,amesema ataakikisha kuwa huduma za jamii zinaboreshwa ikiwa ujenzi wa zahanati,pamoja na shule pia  wakazi wa kalenga watambue kuwa yeye ni mtanzania halali,na si kama ilivyo elezwa awali na chadema na amewataka watanzaia waishi kwa amani na kuto kubaguana.

Kampeni hizo zinatarajiwa kuhitimishwa machi 16,mwaka huu,ambapo kwa mujibu wa ratiba ya Chadema kitakuwa kimefanya kampeni 760 kabla ya wananchi kupiga kura machi 16,mwaka huu.
-ENDS-
 

Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

KITULO FM LOGO

KITULO FM LOGO
Tusikilize masaa 18 kwa siku kupitia masafa ya 97.0 FM ukiwa wilayani Makete mkoani Njombe na maeneo ya jirani

WASOMAJI WETU

KUMBUKUMBU YA HABARI ZETU

 

Copyright © 2013. KITULOFM BLOG - Haki zote zimehifadhiwa
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inawezeshwa na Kitulo Fm