Home » » MAJENGO ya zamani ya serikali na ofisi za umma yametajwa kuwa ni miongini mwa changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu kutokana na ujenzi

MAJENGO ya zamani ya serikali na ofisi za umma yametajwa kuwa ni miongini mwa changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu kutokana na ujenzi

Written By kitulofm on Tuesday, 25 February 2014 | Tuesday, February 25, 2014


Na Amina Mbwambo.

Hai

MAJENGO ya zamani ya serikali na ofisi za umma yametajwa kuwa ni miongini mwa changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu kutokana na ujenzi wake kuto zingatia mahitaji ya kundi hilo ambalo lilisahaulika wakati wa ujenzi wa miundombinu ya majengo hayo.

Hayo yalibainishwa hivi karibuni na makamu mwenyekiti wa chama cha wasioona Tanzania (TLB) Robert Bundala wakati wa warsha ya uandaaji wa mchakato wa mpango mkakati wa chama cha wasioona wilaya ya Hai iliyofanyika Papaa Motel.

Bundala alisema suala la majengo ambayo si rafiki kwa watu wenye ulemavu ni changamoto kubwa sana na kwamba baada ya kutungwa kwa sheria namba 9 ya mwaka 2010 ya watu wenye ulemavu hili jambo limezingatiwa kwa kiwango kikubwa japokuwa haijaanza kufanya kazi.

"Desemba 3 tulipokuwa na siku ya watu wenye ulemavu Duniani mh Rais Kikwete alituthibitishia kwamba hili wameshaelekezwa wahandisi wote wa halmashauri zote nchini na hata wale binafsi kuanzia sasa ni marufuku kwa jengo lolote la umma na binafsi kujengwa bila kuwepo na miundombinu inayohusisha watu wenye ulemavu "alisema Bundala.

Kuhusu suala la maandishi ya nukta nundu Bundala alisema vifaa vinavyotumika kwa ajili ya maandishi hayo ni ghali sana hasa hapa nchini na kwamba TLB tayari imeanza mahusiano mazuri na wafanyabiashara baada ya kuzungumza nao .

"Baada ya kuzungumza na wafanyabiashara wa maduka ya shajala ni kwamba sasa hivi vifaa kwa ajili ya maandishi ya nukta nundu pamoja na fimbo nyeupe vinapatikana kwa hiyo suala linalobaki hapa ni uongozi wa chama katika ngazi ya wilaya  kuwasiliana na makao makuu kuweza kupata vifaa hivi."alisema Bundala.

Aidha Bundala alitoa wito kwa halmashauri ya wilaya ya Hai,ambayo kwanza inapaswa kuzingatia ambayo ni kutambua uwepo wa watu wenye ulemavu ,mahitaji ya walemavu pamoja na kujumuisha mahitaji ya wenye ulemavu wakati wa mipango ya bajeti .

"Halmashauri inapaswa itambue kujumuisha mahitaji ya watu wenye ulemavu wakati wa uwekaji wa mipango ya bajeti vinginevyo kundi hili linaweza kujikuta linaachwa nyuma ,linapata shida ,wanateseka kwa sababu tu halishirikishwi"alisema Bundala.

Alisema sula jingine ambalo ameona ni dosari ni kutokuwepo kwa shule maalumu ya serikali na Chuo cha maendeleo kwa kundi la watu wenye ulemavu jambo ambalo linaashiria kuwepo kwa dalili ya kutengwa kwa watu wenye ulemavu hata chuo cha maendeleo ya jamii pia hakuna.

"Hii halmashauri ina kata 14 hivyo basi ina kila sababu ya msingi ya kuwa na shule ambayo ita accommodate(tosheleza) masuala mengi ya watu wenye ulemavu wa kuona kwa sababu hata wale waliochelewa kupata elimu watapata fursa ya kujifunza maandishi ya nukta nundu na kupata elimu katika shule hizo."alisema Bundala.
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

KITULO FM LOGO

KITULO FM LOGO
Tusikilize masaa 18 kwa siku kupitia masafa ya 97.0 FM ukiwa wilayani Makete mkoani Njombe na maeneo ya jirani

WASOMAJI WETU

KUMBUKUMBU YA HABARI ZETU

 

Copyright © 2013. KITULOFM BLOG - Haki zote zimehifadhiwa
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inawezeshwa na Kitulo Fm