Kushoto ni Askofu mstafu wa Dayosisi ya kusini Kati Dkt. Solomon Swalo na Kulia ni Askofu wa KKKT wilayani Makete
Kundi la wachungaji wakielekea Kanisani
Kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri wilaya Makete,Katikati ni Mkuu wa wilaya ya Makete na Kulia ni aliyekuwa Msaidizi wa askofu msataafu Mch.Manyewa
Wanakwaya wakiimba nyimbo
Kwa habari,picha zote na Edwin Moshi Makete
Wananchi wilayani Makete Mkoani Njombe wametakiwa kujijengea utaratibu wa
Kujisomea Vitabu Mbalimbali kwani ni
Njia Moja wapo yakuongeza Maarifa.
Kauli hiyo imetolewa na Askofu mstafu wa Dayosisi ya kusini Kati Dkt.
Solomon Swalo katika Tafrija ya kumpongeza baada ya kutunukiwa shahada ya
Uzamivu (PHD) iliyofanyika jana Bulongwa wilayani hapa
Dkt. Swalo ambaye pia ni mwandishi mahili wa vitabu amesema amekuwa
akiandika vitabu mbalimbali kwa ajili ya kuweka kumbukumbu ya vizazi vilivyopo
na vijavyo lakini hakuna wasomaji wa vitabu hivyo.
Akizungumza kwa niaba ya Serikali Mkuu wa Wilaya ya Makete Josephine
Matiro Amesikitishwa na tabia ya Baadhi ya watu ya kuto kupenda kusoma Vitabu na
kuwataka wananchi kuanza kujisomea.
Matiro amesema kuwa serikali ipo pamoja na kanisa ili kuleta maendeleo
Hivyo anaimani mchango wa Askofu Mstaafu Dk. Swalo bado Unahitajika sana katika Jamii.
Katika Hatua nyingine kanisa limempa Hati ya Jengo Askofu Dk Swalo kwa ajili
ya kuuzia Vitabu lililopo Eneo la Namanga Bulongwa.
Tukio Hilo la Kumpongeza Dk Swalo limehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa
Serikali,kanisa pamoja na wananchi.
0 comments:
Post a Comment