Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Godfrey Sanga amepandishwa kizimbani mach 2014 katika mahakama ya wilaya Makete Mkoani Njombe kwa tuhuma ya kumpa mimba mwanafunzi.
Akielezea
kutokea kwa tukio hilo mwendesha mashtaka wa polisi Bw,gosbet
komba mbele ya hakim wa wilaya mh, j, s.
obas amesema tukio hilo limetokea februali 2 mwaka huu majira ya saa moja usiku
katika kata ya tandala.
Bw.Komba amesema mtuhumiwa huyo amefanya
tukio hilo la
kumpa mimba mwanafunzi na kumsababishia kukatisha masomo yake.
Hata
hivyo mshtakiwa huyo amekana shitaka linalo mkabili na dhamana yake iko wazi
kwa wadhamini wawili wa kuaminika na sh. Milioni moja kwa kila mmoja na
mtuhumiwa huyo yuko nje kwa dhamana mpaka kesi yake itakapo tajwa tena aprili
04 mwaka huu.
Jina
la mwanafunzi huyo limehifadhiwa,
0 comments:
Post a Comment