Home » » AUWAWA KWA MAWE KISHA KUCHOMWA MOTO KWA WIZI WA PIKIPIKI WILAYANI KAHAMA

AUWAWA KWA MAWE KISHA KUCHOMWA MOTO KWA WIZI WA PIKIPIKI WILAYANI KAHAMA

Written By kitulofm on Tuesday, 25 March 2014 | Tuesday, March 25, 2014

Baadhi ya wananchi wa mji mdogo wa Kagongwa wilayani Kahama wakiangalia mwili wa marehemu
 
Kijana mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 25-30 ameuawa kwa kupigwa mawe kisha kuchomwa moto na wananchi wenye hasira kali baada ya kukamatwa na pikipiki ya wizi Katika kijiji cha kagongwa Wilayani Kahama mkoani Shinyanga. 
Tukio hilo limetokea jana majira ya saa nane Mchana mara baada ya marehemu kuiba Pikipiki hiyo yenye no T634 CNK Aina ya SanLG mali ya Patrick Seba mkazi wa Nyahanga Mjini Kahama ambayo imeibiwa jana Asubuhi Maeneo ya shule ya Kahama Musilim ikiwa imeegeshwa na dereva wake aitwaye Shija Zacharia.

Kwa mujibu wa Mmiliki wa pikipiki hiyo Bwana Seba Ameiambia redio Kahama fm Kuwa alipewa taarifa na dereva wake ambpo aliamua kutoa tarifa ya upoteza pikipiki hiyo kwa waendesha bodaboda wa mjini Kahama na Kagongwa.
Amesema wakati anatoka Kagongwa kutoa taarifa ndipo akakutana na vijana wawili ambao walikuwa wanaiendesha pikipiki hiyo kuelekea Kagongwa ambapo aliamua kuwafuatilia na kwamba aliwapata katika kijiji hicho.

Baada ya kuwasogelea aliizima pikipiki hiyo kwa kutumia remote kwani wakati inaibiwa ilikuwa imezimwa kwa kutumia Remote ambapo walianguka china na Kuanza kukimbia huku wananchi wakaanza kumshambulia mmoja kwa mawe hadi kumuua huku mwingine akifanikiwa kukimbia kusikojulikana.
Hata hivyo jeshio la Polisi wilayani Kahama limedhibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba mwili wa marehemu ulipelekwa kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifdadhia maiti kwenye hospitali ya Wilaya ya kahama.
Kwa takribani miezi Miwili na Nusu sasa watu wa wanne wameuawa kwa kuchomwa na moto katika kijiji hicho kwa madai kuwa wamechoshwa na kukithiri kwa wimbi la wizi katika Kijiji hicho na maeneo jirani. 
chanzo: Dunia Kiganjani 
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

KITULO FM LOGO

KITULO FM LOGO
Tusikilize masaa 18 kwa siku kupitia masafa ya 97.0 FM ukiwa wilayani Makete mkoani Njombe na maeneo ya jirani

WASOMAJI WETU

KUMBUKUMBU YA HABARI ZETU

 

Copyright © 2013. KITULOFM BLOG - Haki zote zimehifadhiwa
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inawezeshwa na Kitulo Fm