Na Eleuteri Mangi- MAELEZO
Serikali
imesema utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirishia gesi
asilia kutoka Mtwara hadi Dar es salaam unaenda vizuri kulingana na
ratiba yake na utakamilika kwa wakati.
Kauli hiyo
imetolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue alipotembelea
kituo cha kufua umeme kwa kutumia gesi asilia kinachojengwa Kinyerezi
wakati akihitimisha ziara yake ya siku mbili ya kukagua mradi wa ujenzi
wa bomba la gesi jijini Dar es salaam.
Balozi Sefue alisema kuwa ni vema kufanyakazi kwa uadilifu na hakuna mchezo, kazi ikitolewa ikamilike kwa wakati.
"Tujenge
uchumi wa nchi yetu kwa kutumia umeme wa uhakika, uhakika huo unatokana
na gesi asilia tuliyonayo" alisisitiza Balozi Sefue.
Akifafanua
zaidi Balozi Sefue alisema kuwa kugunduliwa kwa gesi nchini kumeanza
kuleta manufaa mengi ikiwamo wanafunzi kupata udhamini katika masomo yao
katika ngazi mbalimbali za elimu, shule zimejengwa, wananchi wa mikoa
ya Lindi na Mtwara wanapata maji safi na kupata ajira mbalimbali.
Naye
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi alisema kuwa
fedha za ujenzi wa kituo cha kinyerezi I na ujenzi wa vituo vingine vya
kinyerezi II, III na IV, zinatolewa na Serikali ya Tanzania kwa
kushirikiana na wahisani.
Fedha za ujenzi wa kituo
cha Kinyerezi I zimetolewa na Serikali kupitia TANESCO na ujenzi wa
kituo cha kinyerezi II fedha itatokana na ubia kati ya Serikali ya
Tanzania na Japani , wakati ujenzi wa kinyerezi III na IV fedha
zitatokana na kuingia ubia kati ya Serikali na kampuni ya Kichina.
Alimhakikishia
Balozi Sefue kuwa Wizara yake ipo tayari kupokea maelekezo na ushsuri
kutoka ngazi za juu za Serikali katika kutekeleza mradi huo wa ujenzi wa
bomba la gesi asilia na hatimaye kuongeza uzalishaji wa umeme ili
kujenga uchumi wa kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.
Mkurugenzi
Mkazi wa Mradi huo Bw. Shaun Moore, alimweleza Katibu Mkuu Kiongozi na
msafara wake kuwa maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho yanaendelea vizuri
kutokana na kampuni hiyo kufanya kazi kwa ushirikiano mzuri na kampuni
za kitanzania zilizochukua kandarasi tofauti za ujenzi wa kituo hicho
ambapo takribani asilimia 98 ya kandarasi na wafanyakazi ni kutoka
kampuni za kitanzania.
Ziara hiyo ilianzia mikoa
ya Mtwara, Lindi, Pwani na kuhitimishwa Dar es salaam ambapo Katibu Mkuu
Kiongozi aliambatana na Makatibu Wakuu 12 wa Wizara zinzotekeleza
Mpango wa Mataokeo Makubwa Sasa (BRN).
kwa kutumia gesi asilia kinachojengwa Kinyerezi wakati akihitimisha ziara yake
ya siku mbili ya kukagua mradi wa ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi
Mkuu TANESCO Felchesmi Mramba akimweleza Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni
Sefue na msafara wake hatua zilizofikiwa kwenye ujenzi wa kituo cha kufua umeme
kwa kutumia gesi asilia kinachojengwa Kinyerezi wakati akihitimisha ziara yake
ya siku mbili ya kukagua mradi wa ujenzi wa bomba la gesi jijini Dar es salaam.
Moja ya eneo la kituo cha Kenyerezi I ambapo inajengwa mitambo ya kufua umeme kwa
kutumia gesi asilia.
Picha
zote na Eleuteri Mangi- MAELEZO
CHANZO:MICHUZI BLOG
0 comments:
Post a Comment