Home » » OBAMA AIONYA URUSI KWA VIKWAZO ZAIDI

OBAMA AIONYA URUSI KWA VIKWAZO ZAIDI

Written By kitulofm on Wednesday, 26 March 2014 | Wednesday, March 26, 2014

Rais Obama anatarajiwa kusisitiza umuhimu wa usalama Marekani na Ulaya

Rais Obama yuko mjini Brussels ambapo atakutana na viongozi wa muungano wa Ulaya na shirika la kujihami la NATO, kuzungumzia mzozo wa Ukraine.

Kwenye hotuba muhimu kuhusu sera Rais Obama anatarajiwa kusisitiza umuhimu wa usalama wa Marekani na nchi za Ulaya na pia kuonya Urusi dhidi ya kukiuka sheria za kimataifa.

Akizungumza mjini the Hague kabla ya kuelekea Brussel Rais Obama ameitaja hatua ya Urusi kutwaa eneo la Crimea kutoka kwa Ukraine kama ishara ya udhaifu.

Hatahivyo amesema bado kuna nafasi ya Urusi kusuluhisha mzozo huo kwa njia ya amani la sivyo ikabiliwe na vikwazo zaidi vya kiuchumi.

 Amesema japo huenda vikwazo hivyo vikaathiri uchumi wa dunia,Urusi ndio itakayoathirika zaidi.


Mkutano huo pia unatarajiwa kuzingatia maswala ya kibiashara na pia wasiwasi kwamba Marekani imekuwa ikichunguza kisiri shuguli za washirika wake kutoka nchi za Ulaya.
CHANZO:BBC
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

KITULO FM LOGO

KITULO FM LOGO
Tusikilize masaa 18 kwa siku kupitia masafa ya 97.0 FM ukiwa wilayani Makete mkoani Njombe na maeneo ya jirani

WASOMAJI WETU

KUMBUKUMBU YA HABARI ZETU

 

Copyright © 2013. KITULOFM BLOG - Haki zote zimehifadhiwa
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inawezeshwa na Kitulo Fm