Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Gabriel Tuppa (aliyeshika karatasi)
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya
Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Hawa Ghasia
kufuatia kifo cha Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Gabriel Tuppa, aliyefariki
Machi 25, 2014 katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime.
Pokea rambirambi zangu za dhati na masikitiko makubwa kufuatia kifo
cha, John Gabriel Tuppa. Ni huzuni kubwa na pigo kwa Serikali na hasa
kwa Watendaji wenzake mkoani Mara ambao alikuwa akifanya nao kazi.
Marehemu John Gabriel Tuppa amefariki leo tarehe 25 Machi,2014 katika
Hospitali ya Wilaya ya Tarime.
Rais pia amemwomba Ghasia amfikishie salamu za pole kwa Mke wa
Marehemu, Watoto na Familia ya Marehemu kwa kuondokewa na kipenzi chao.
Rais amesema, anaelewa machungu wanayoyapitia katika kipindi hiki kigumu
kwani wamepoteza nguzo imara waliyokuwa wakiitegemea katika maisha yao.
“Hakika tumempoteza kiongozi mchapakazi ambaye amekuwa akijituma na
kuwatumikia Wananchi wake hadi dakika za mwisho za uhai wake. Pengo
aliloliacha Marehemu Tupa haliwezi kuzibika kamwe lakini hatuna budi
kumwombea kwa Mwenyezi Mungu kuipumzisha roho ya Marehemu mahali pema
peponi,” Amina.
Taratibu na maandalizi ya mazishi zinafanywa kwa ushirikiano wa
Familia, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara na Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI.
Marehemu Tupa alizaliwa tarehe 01 Januari, 1950 na katika enzi za
uhai wake amewahi kuongoza Wilaya za Chunya, Mwanga, Bukoba, Muleba na
Dodoma kabla ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara Mwaka 2011. Ameacha
Mke na watoto watano.
0 comments:
Post a Comment