Picha na Maktaba,Habari na Fadhili Lunati
Utekelezaji wa miradi ya usambazaji wa maji makete mjini kata ya Iwawa wilayani Makete Mkoani Njombe unaendelea vizuri hadi hivi sasa
Taarifa hiyo imetolewa mapema leo na Meneja wa Mamlaka
ya maji Makete mjini Bw.Yonas Ndomba kwa waandishi wa habari ambapo ameeleza
kuwa hadi kufikia sasa miradi hiyo imetekelezwa kwa kiasi kikubwa hadi kufikia
asilimia 90
Bw.Ndomba amesema kuwa usambazaji wa maji hayo
itawasaidia sana wakazi wa Makete mjini kwani
hata wale waliokuwa wanalalamika kutopata huduma ya maji kwa mda wote hivi sasa
tatizo hilo
linapungua
Pia amewaomba wakazi wa Makete mjini wanaotumia huduma
ya maji na kwa kila mmoja mmoja kutoa taarifa katika mamlaka husika pindi
wanapokuwa wamebaini eneo lolote ambalo Bomba la kupitisha maji limepasuka
kutoa taarifa mapema ili eneo hilo
liweze kudhibitiwa mapema na kupunguza adha ya upatikanaji wa maji
Bw.Ndomba amewataka wateja wa maji kulipia bili zao
kwa wakati kwani bili huwa zinatolewa mapema wakifanya hivyo basi watajiepusha
na usumbufu ambao huenda ukajitokeza
0 comments:
Post a Comment