
Mkuu wa Polisi Kenya amesema bado hawajafutilia mbali kwamba lilikua
shambulio la kigaidi ambapo kwa mujibu wa Erick Ponda ambae ni mwandishi
wa habari wa DW Mombasa alieongea akisema mpaka March 24 2014 jioni watu 59 walikua wamekamatwa na Polisi kwenye msako wakituhumiwa kuhusika na shambulio hilo.
Wakati huohuo, mtoto ambae bado kichwani kwake kuna risasi aliyopigwa
kwenye shambulio hilo amepelekwa kwenye hospitali ya binafsi kwa
matibabu maalum kwa sababu anahitaji kufanyiwa upasuaji ili kuokoa
maisha yake.
Mama mzazi wa mtoto huyu alifariki kwenye hili shambulio hivyo kwa
sasa mtoto yuko na ndugu wa mama yake ambae namkariri akisema ‘haendelei
vizuri manake amekua akinisumbua hawezi kulala, ana maumivu makali sana
kichwani kutokana na hiyo risasi ndani ya kichwa’
Viongozi wa kidini wakiongozwa na Askofu Julius Atsango wamewataka
wenzao wa dini ya kiislamu kuisaidia serikali kuwakamata wanaosingizia
dini kutekeleza mashambulizi.
CHANZO:EDDY BLOG
0 comments:
Post a Comment