Kutokana
na mvua zinazoendelea kunyesha wilayani Makete zimeharibu barabara hii
kama unavyoona, hapa ni kijiji cha Isapulano ambapo mvua imeharibu
barabara hii kiasi cha kusababisha mabasi na malori kubadilisha njia na
kupita kijiji jirani cha Ivalalila, hapa yanapita magari madogo tu tena
yenye 4 wheel ambao nayo yanapita kwa tabu.
Hali
hii amekutana nayo mwandishi wetu wakati akielekea kwenye uzinduzi wa
wiki ya chanjo wilaya ya Makete ambayo imezinduliwa kiwilaya katika
kijiji cha Isapulano..(Picha na Edwin Moshi)
0 comments:
Post a Comment