Nchi kadhaa za Afrika magharibi zimepania kuipiga vita homa hatari ya
Ebola iliyoangamiza maisha ya zaidi ya watu 80 nchini Guinea,siku moja
tu baada ya homa hiyo kuripotiwa Mali,baada ya Liberia na Sierra Leone.
Mali nchi inayopakana na Guine imesema jana usiku,kadhia tatu za homa ya
Ebola zimegunduliwa nchini humo na walioambukizwa kuwekwa karantini.
"Watu hao watatu hali yao hivi sasa ni nzuri,hakuna tena dalili ya
kuvuja damu-mojawapo ya ishara za homa ya Ebola" amesema waziri wa afya
na usafi wa jamii Ousmane Koné.Kwa mujibu wa Dr. Omar Sangaré,wa idara
ya afya watu hao wote watatu ni raia wa Mali waliokuwa wakifanya kazi
katika eneo la mpakani kati ya Mali na Guine.
Serikali ya Mali imewaonya raia wasifike katika maeneo ya maambukizi.
Nchi iliyoathirika zaidi ni Guine ya Conacry ambako homa hiyo
inayosababisha watu kuvuja damu imeshaangamiza maisha ya watu 86 toka
jumla ya watu 137 walioambukizwa tangu january mwaka huu-wengi wao ni wa
kutoka eneo la kusini-kwa mujibu wa ripoti ya serikali.
Ishara za matumaini mema
Kadhia 45 kati ya hizo zimethibitishwa kuwa ni za homa ya
Ebola,maradhi hatari yanayoambukiza na ambayo hadi wakati huu hayana
tiba wala chanjo."Lakini wagonjwa wawili waliokuwa wamewekwa karantini
wamethibitishwa wamepona mjini Conacry"-serikali imesema.
Matumaini finyu yamechomoza katika wakati ambapo shirika la madaktari
wasiokuwa na mipaka ,linaloendesha shughuli zake nchini Guine
linazungumzia juu ya "mambukizi yasiokuwa na mfano".
0 comments:
Post a Comment