CHANZO:BBC
Baadhi ya watafiti wa masuala ya kielimu nchini
Tanzania wamesema mgawanyo mbaya wa walimu katika ajira mpya ni moja ya
mambo yanayokwamisha maendeleo ya kielimu ikiwemo kushuka viwango vya
ufaulu kwa wanafunzi katika shule za msingi nchini humo.
Shirika lisilo la kiserikali la haki elimu
limesema utafiti wake umebaini kuwa mikoa ya kanda ya magharibi nchini
humo na ile iliyopo ziwa Victoria haijafikia malengo ya kitaifa ya idadi
ya walimu katika kila shule
Katika
ripoti hiyo ya utafiti wa shirika la Hakielimu, imeeleza kwamba
mgawanyo wa walimu wapya haujalenga uhaba wa walimu uliopo.
Shirika hilo linasema kuwa baadhi ya mikoa
iliyopokea mwalimu mmoja kwa kila wanafunzi 37, imeongezwa walimu jambo
ambalo sio sawa kwa sababu baadhi ya mikoa haina walimu wa kutosha na
hilo linapaswa kuzingatiwa.
Haki elimu wanasema sababu hizo ni baadhi ya
mambo yanayochangia ufaulu duni , ambapo kwa kipindi cha miaka minne
iliyopita ufaulu kwa shule za msingi umekuwa ni wastan wa asilimia 60
hadi 40 tu.
Limeongeza kwamba walimu wanataka kuishi katika
mikoa ya karibu na hivyo kufanya kila wawezali kuwashawshi wadau
kutowapeleka mikoa ya mbali.
Hata hivyo ripoti hiyo imetofautisha walimu wa
sasa na wale wa miaka iliyopita. Linasema kuwa walimu wa zamani walikuwa
na haiba, uzalendo na kujitolea kufanya kazi na pia walithaminiwa sana
na jamii lakini leo kazi ya ualimu imekuwa kazi ya ilimradi
Baadhi ya mikoa nchini Tanzania imebuni mbinu
zinazoweza kuwavutia walimu ili wafanye kazi katika maeneo yao kutokana
na maeneo hayo kukosa walimu kwa miaka mingi mfululizo kutokana na
mazingira duni ya kazi
0 comments:
Post a Comment