Baadhi ya walimu wakiwa katika picha ya pamoja
Picha na Furahisha Nundu
Uongozi
wa shule ya Msingi Ibaga kata ya Mang’oto wilaya ya Makete Mkoani Njombe
umeilalamikia serikali kutoangalia suala la ukuzaji wa taaluma katika shule
hiyo
Akizungumza
na Kitulo fm Mkuu wa shule hiyo Mwl.Ambonwilo Chengula amesema kuwa shule yake
haijapokea walimu wa mazoezi kwa muda mfupi ilihali shule za jirani zimepata
walimu hao
Shule
hiyo inajumla ya walimu 8 ambapo mwalimu mmoja kati ya hao anasumbuliwa n a
maradhi na mungine yupo masomoni hivyo kuna changamoto kubwa ya kuhakikisha
kuna ukuaji wa taaluma shuleni hapo
Amesema
Shule hiyo inazaidi ya wanafunzi 180 kiwango ambacho ni kikubwa ukilinganisha
na walimu sita tu wanaofanya kazi kwa wakati huu pamoja na walimu wapywa
waliopelekwa
Pia
Mkuu huyo amesema kuwa tatizo hilo limechangiwa hasa na tatizo la ubovu wa
miundombinu pamoja na kutokuwepo kwa mawasiliano ikiwa endapo serikali
italitilia maanani suala la miundombinu na mawasiliano ni jambo ambalo
litasaidia walimu kupatikana na kuongeza kiwango cha ukuaji wa elimu shuleni
hapo
0 comments:
Post a Comment