Vijana wakimbizi wanaoishi katika kambi kubwa zaidi
ya wakimbizi duniani, nchini Kenya, Dadaab wamewatumia barua za kuwapa
matumaini watoto wanaokumbwa na vita nchini Syria, ambao wamelazimika
kutoroka vita na kukimbilia nchi jirani.
Wakimbizi hao wanaishi Dadaab Kaskazini mwa
Kenya. Ni makao kwa wakimbizi 400,000 wengi wao waliotoroka vita, njaa
na ukame nchini Somalia.
Vita hivyo vimekuwa vikiendelea kwa miaka 23 sasa.
Shirika la misaada la kimataifa la Care
International, ambalo hutoa misaada kwa wakimbizi hao, liliandaa mpango
wa kuandikiana barua kati ya watoto hao na wale wa Syria wanaoishi
katika kambi ya wakimbizi ya Amman nchini Jordan.
0 comments:
Post a Comment