Home » » JELA KWA KUMKATA KICHWA MPENZI WAKE

JELA KWA KUMKATA KICHWA MPENZI WAKE

Written By kitulofm on Thursday, 17 April 2014 | Thursday, April 17, 2014

Mwanamume aliyemuua kwa kumkata kichwa mpenzi wake amepatikana na hatia ya mauaji nchini Uingereza

Aras Hussein alimkata kichwa mwanafunzi mwenye umri wa miaka 18 Reema Ramzan nyumbani kwake katika mtaa wa Sheffield mwezi Juni kabla ya yeye mwenyewe kujidunga kisu kifuani mwake Aras amehukumiwa kifungo cha maisha jela.

Hussein, alikiri kumuua mpenzi wake baada ya kuzozana ingawa awali alikana madai ya mauaji.

Mwili wa Ramzan ulipatikana katika sehemu ya jikoni ya nyumba ya Hussein tarehe nne mwezi Juni.

Polisi walipigiwa simu na mpita njia mmoja aliyemuona Hussein akitembea uchi nje akiwa na damu katika mwili wake.
Madaktari walipojaribu kumsaidia kwa kumpa huduma ya dharura aliwauliza kwa nini walikuwa wanataka kumsaidia wakati amemuua mtu nyumbani kwake.

Alipoulizwa kwa nini alifanya hivyo, akajibu kuwa hajui.
Mahakama ilisikia ambavyo msichana huyo alidungwa kisu kifuani na kisha kukatwa kichwa chake.

Pia mikono yake ilikuwa na alama za kuonyesha kuwa alijaribu kujikinga kutokana na kushambuliwa na mpenzi wake
Kiongozi wa mashitaka aliambia mahakama kuwa marehemu Ramzan bado alikuwa hai wakati Aras alipoanza kumkata koo kwa kutumia nguvu.

Wakati kesi ilipokuwa inaendelea , mahakama iliambiwa na familia ya Ramzan kuwa hawakupenda uhusiano kati ya wawili hao.
Siku ya kuuliwa kwake, alikuwa amekwenda nyumbani kwa Aras akiwa na Pasi yake ya usafiri pamoja na kitita kikubwa cha pesa


Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

KITULO FM LOGO

KITULO FM LOGO
Tusikilize masaa 18 kwa siku kupitia masafa ya 97.0 FM ukiwa wilayani Makete mkoani Njombe na maeneo ya jirani

WASOMAJI WETU

KUMBUKUMBU YA HABARI ZETU

 

Copyright © 2013. KITULOFM BLOG - Haki zote zimehifadhiwa
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inawezeshwa na Kitulo Fm