Mawimbi makali na hali mbaya ya hewa baharini imetatiza
juhudi za utafutaji na uokoaji wa takriban watu mia tatu baada ya feri ya
abiria kuzama katika pwani ya Korea Kusini.
Juhudi za uokoaji zikiwa zinaendelea
Watu
tisa wamethibitishwa kuaga dunia katika mkasa huo.
Wengi
wa abiria kwenye meli hiyo walikuwa ni wanafunzi wa shule ya upili. Takriban
watu mia moja sabini wameokolewa. Kapteni wa jeshi la wanamaji la Marekani
Heidi C. Agle anashiriki katika operesheni ya uokoaji.
Ameiambia
BBC kuwa maandalizi yanafanywa kupeleka mtambo wa kuinua chombo hicho.
Wakati
huohuo Rais Park Geun-hye, amewataka waokozi kuharakisha juhudi zao za
kuwatafuta manusura wa ajali hiyo.
Rais
Park -- ambaye amejionea meli hiyo mwenyewe, amesema kuwa kila dakika ni muhimu
katika kuhakikisha kuwa manusura wanapatikana.
Wapiga
mbizi wamekuwa wakikabiliana na mawimbi makali kujaribu kukifikia chombo hicho
kilichozama hapo jana.
Duru
zinasema kuwa meli hiyo ilipoteza mwelekeo huku baadhi ya familia za waathriwa
zikihoji mwenendo wa nahodha wa meli.
Hata
hivyo nahodha huyo Lee Joon-seok aliomba msamaha na kusema ana majuto tele na
kuwa hata hajui la kusema.
Dauru
zinseama kuwa miongoni mwa wliofariki ni wanafunzi wanne wenye umri wa miaka 17
na mwaliamu wao mwenye umri wa miaka 25 pamoja na mfnyakazi mmoja wa meli hiyo.
Wengine
wlaiofariki bado hawajatajwa.
Takwimu
za hivi karibuni zinasema kuwa wtu 475 walikuwa kwenye meli hiyo huku 287
wakiwa bado hawajapatikana.
CHANZO:BBC
0 comments:
Post a Comment