Home » » KINANA AKUMBANA NA MAJANGA BARABARA YA NKASI MKOANI RUKWA

KINANA AKUMBANA NA MAJANGA BARABARA YA NKASI MKOANI RUKWA

Written By kitulofm on Thursday, 3 April 2014 | Thursday, April 03, 2014

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akimueleza jambo Mbunge wa jimbo la Nkasi Kaskazini,Mh.Ali Mohammed Kessy,walipokuwa wakitembea kwa miguu kufuatia msafara huo kukumbana na changamoto ya barabara mapema jana jioni katikati ya Msitu wa hifadhi ya wilaya ya Nkasi.Ndugu Kinana na Msafara wake ulikuwa umetoka kijiji cha Namanyere kuelekea kijiji cha Mwampemba kusikiliza matatizo ya Wananchi na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo iliyopangwa kutekelezwa kwenye Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2010.

Barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 100,lakini iliwachukua zaidi ya masaa 12 kwenda na kurudi kutokana na ubovu wa barabara.Ndugu Kinana yuko Mkoani Rukwa,Katavi na Kigoma kwa ziara ya siku 21 ya kuimarisha Chama cha CCM,kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo kiwemo na kuzisikiliza kero mbalimbali za wananchi.
Ndugu Kinana akishiriki kuweka mawe sehemu korofi,angalau kusaidia Lori hilo pichani lililolala ndani ya msitu huo kwa siku mbili,wapite nae msafara wake uweze kuendelea na safari.
Sehemu korofi ya Barabara ikiwekwa sawa ili lori lipite na kisha msafara nao uweze kupita,lakini hata hivyo zilitumika juhudi kubwa kuvusha msafara wa Kinana na hatimae kuendelea na safari ya kuelekea kijiji kingine.
Ndugu Kinana akizungumza na baadhi ya Wanahabari aliokuwa ameambatana nao kwenye msafara wake,baada ya magari kunasa kutokana tatizo la barabara.
Wanahabari waliokuwa kwenye msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana wakiwa hoi kabisa,wakisubiri kudra za Mwenyezi Mungu,msafara wa magari yao yanasuliwe na kuendelea na safari.Picha hii imepigwa na Katibu Mkuu,Ndugu Kinana.
Hali ilikuwa tete mnoo,kipande cha kilometa mia kinapitika kwa zaidi ya masaa sita, kutoka kijiji kimoja kwenda kingine..
ccm 1
Ilikuwa ni shughuli nzito katika msafara wa Ndugu Kinana, barabara ni mbovu kupita maelezo.
 
Kila mmoja akipumua kivyake,baada ya kuvuka salama sehemu korofi ya barabara.
 
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana (alinaerusha jiwe) akishiriki kuziba sehemu korofi kwa mawe,ili msafara uweze kupita.
Pichani kulia ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndug Kinana akiongoza kuvuka sehemu korofi ya barabara kwa miguu,huku madera wakipiga hesabu zao namna ya kupita.

PICHA NA MICHUZIJR-MICHUZI MEDIA GROUP-NKASI RUKWA.
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

KITULO FM LOGO

KITULO FM LOGO
Tusikilize masaa 18 kwa siku kupitia masafa ya 97.0 FM ukiwa wilayani Makete mkoani Njombe na maeneo ya jirani

WASOMAJI WETU

KUMBUKUMBU YA HABARI ZETU

 

Copyright © 2013. KITULOFM BLOG - Haki zote zimehifadhiwa
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inawezeshwa na Kitulo Fm